Friday, October 30, 2015

DK.MAGUFULI AWASHUKURU WATANZANIA WOTE.

Dk. John Pombe Magufuli rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano (5) akiwashukuru watanzania wote waliompatia Ushindi kwenye uchaguzi wa Rais, uliofanyika tarehe 25.
Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli na Makamu wake Mteule, Mama Samia Suluhu Hassan  wakionyesha Vyeti walivyokabidhiwa na Jaji Mstaafu Damian Lubuva wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi mara baada ya kushinda kiti cha Urais kwenye uchaguzi uliofanyika tarehe 25.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe joseph Magufuli nje ya Makao Makuu ya CCM jijini Dar es Salaam.



Mh. Rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli akimtambulisha mkewe Mama Janeth Pombe Magufuli mbele ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano Dr. John Pombe Joseph Magufuli, Mama Janeth John Magufuli Katika Picha

 Posted by Emman W.

DK. JOHN POMBE MAGUFULI AKABIDHIWA CHETI

Dk. John Pombe Magufuli akiyonyesha cheti cha ushindi wa Urais, baada ya kukabidhiwa cheti hicho na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Jaji Mstaafu Damian Lubuva akimkabidhi Makamu wa Rais Mteule, Mama Samia Suluhu Hassan hati ya Ushindi.


MH.JAKAYA PICHA YA PAMOJA NA DK. MAGUFULI

Mh. Jakaya Kikwete na Rais mteule wa Jamhuli ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja

Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva  na viongozi mbali mbali wa vyama vya kisisa.

Rais Mteule wa Tanzania, Mh. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na viongozi mbali mbali wa dini zote.

 Posted by Emman W

Saturday, October 24, 2015

MAFULIKO YA MAGUFULI MWANZA



Dk. John Pombe Joseph Magufuli akiwasili uwanja wa CCM Kirumba tayari kwa kuhutubia mkutano wa kufunga kampeni za CCM jijini Mwanza. Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi leo amehitimisha kampeni zake jijini Mwanza ambapo maelfu ya wananchi walihudhuria. Katika mkutano wa kampeni za chama cha cha CCM, zimehudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete pamoja na mgombea mwenza wa urais Samia Suluhu Hassan.
Dk. John Pombe Joseph Magufuli katika Jukwaa la viwanja wa CCM Kirumba akihutubia mkutano.
Rais Jakaya Kikwete akimnadi Mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe mbele ya wakazi wa jiji la Mwanza waliofurika kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Maelfu ya wananchi wahudhuria mkutano kuhitimisha kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza



 Posted by Emman W