Friday, October 30, 2015

DK.MAGUFULI AWASHUKURU WATANZANIA WOTE.

Dk. John Pombe Magufuli rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano (5) akiwashukuru watanzania wote waliompatia Ushindi kwenye uchaguzi wa Rais, uliofanyika tarehe 25.
Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli na Makamu wake Mteule, Mama Samia Suluhu Hassan  wakionyesha Vyeti walivyokabidhiwa na Jaji Mstaafu Damian Lubuva wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi mara baada ya kushinda kiti cha Urais kwenye uchaguzi uliofanyika tarehe 25.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe joseph Magufuli nje ya Makao Makuu ya CCM jijini Dar es Salaam.



Mh. Rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli akimtambulisha mkewe Mama Janeth Pombe Magufuli mbele ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano Dr. John Pombe Joseph Magufuli, Mama Janeth John Magufuli Katika Picha

 Posted by Emman W.