Saturday, October 24, 2015

MAFULIKO YA MAGUFULI MWANZA



Dk. John Pombe Joseph Magufuli akiwasili uwanja wa CCM Kirumba tayari kwa kuhutubia mkutano wa kufunga kampeni za CCM jijini Mwanza. Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi leo amehitimisha kampeni zake jijini Mwanza ambapo maelfu ya wananchi walihudhuria. Katika mkutano wa kampeni za chama cha cha CCM, zimehudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete pamoja na mgombea mwenza wa urais Samia Suluhu Hassan.
Dk. John Pombe Joseph Magufuli katika Jukwaa la viwanja wa CCM Kirumba akihutubia mkutano.
Rais Jakaya Kikwete akimnadi Mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe mbele ya wakazi wa jiji la Mwanza waliofurika kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Maelfu ya wananchi wahudhuria mkutano kuhitimisha kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza



 Posted by Emman W